WANACHAMA UWAMZ WACHANGIA BENKI YA DAMU

Na Khadija Kalili Michuzi TV

Umoja wa Wajasiriamali zaidi ya 70 wa Mtaa wa Zigua na Mahiwa Kariakoo maeneo ya Msikiti wa Mtoro wamejitolea damu kwaajili ya maandalizi ya kuingilia mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni mwezi 28 Shaban1446 AH kwa lengo la kuchangia Banki ya damu salama ya taifa.

Yamesemwa hayo leo Februari 27 na Katibu wa Umoja wa Wafanyabiashara katika Mitaa ya Mahiwa na Zigua Simba Issa Lichanda

Akizungumza kabla ya kuanza zoezi la utoaaji wa damu Afisa kutoka Kitengo cha Damu Salama Adam. Kweka amesema kuwa anawapongeza waumini wa dini ya Kiislamu kwa sababu wamekuwa mstari wa mbele na wana rekodi ya kuongoza kwa uchangiaji wa damu nchini .

“Nawapongeza ninyi mnawito na takwimu zenu za uchangiaji zipo kwenye benki ya damu” amesema.

Pia nachukua fursa hii kutoa pongezi zangu kwa UWAMZ kwa kuhamasishana na kujitokeza kwa wingi katika kuchangia damu kwani duniani hakujawahi kuwa na mbadala wa amu ieleweke hivyo.

Naye Imamu Mkuu wa Msikiti wa Kwamtoro Ramadhan Abbas uliopo kati ya mitaa ya Mahiwa na Zigua amesema kuwa kutoa damu kwa hiari ni jambo la ibada katika imani huku akitoa wito kwa waumini wake kujitoa kwa ajili ya sadaka hiyo ambayo itawafaa wengine wenye uhitaji kama kima mama wajawazito na wagonjwa wengine walioko mahospitalini wenye kuhitaji damu.

Wakati huohuo

Mwenyekiti wa Mtaa huo Nasra

Mohammed amesema kuwa anatoa wito kwa wakaazi na waafanya biashara wote walioko hata nje ya mitaa hiyo ya Zigua na Mahiwa kujitokeza kuchangia damu kwani hakuna aijuaye kesho yake.

Related Posts