WAZAZI WATAKIWA KUENDELEA KUWAHIMIZA WATOTO KUPENDA ELIMU

Afisa Mkuu Mtaala Mwandamizi wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET), Dk. Joyce Kahambe amewasihi wazazi waendelee kuwahimiza watoto wapende elimu na kufanyia kazi ujuzi wanaojifunza shuleni katika shughuli zao mbalimbali ikiwemo kilimo, ufugaji mziki na mengine hatakama wanataaluma zao.

Hayo ameyasema leo Februari, 28 Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani na Dk.Kihambe wakati wa Mahafali ya saba ya Shule ya Sekondari ya Wavulana Christon amesema TET ni taasisi ya serikali ipo chini ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ambayo inafanya majukumu mbalimbali.

Amesama jukumu la kwanza kuboresha mitaala ya elimu kuanzia awali, shule ya msingi, sekondari na vyuo vya walimu ngazi ya Diploma.Kufuatilia vitu mbalimbali ikiwemo vitabu kutoa mafunzo kwaajili ya mitaala hiyo na inafanya tafiti na kutoa ushauri kuiwezesha shule zote za serikali na binafsi.

“Mitaala hii imeweka msisitizo katika ujuzi hivyo shule ya sekondari ya wavulana Christon hii ipo mbele maana nimeona wanafunzi wanajifunza ujuzi mbalimbali ikiwemo ufugaji, mziki na kilimo Kuhusu utoaji wa mafunzo ya ujuzi hata kwenye mtaala ukiangalia na Sera ya elimu inasisitiza sana ujuzi unamsaidia kuweza kujiajiri na kuajiriwa,” amesema.

Aidha amesema watoto wasione kupata ujuzi mwisho shule ujuzi una levels ujuzi huo wataendelea nao kidato cha tano na masomo ya amali na taasisi zinatambua ujuzi huu,”amesema.

Wazazi kuwasaidia wanafunzi kuendeleza ujuzi waliopata katika shule na kuwatia moyo wanafunzi haya mafunzo sii adhabu kwao ni kuwajengea uwezo na kuwa msingi katika maisha yao.

Naye Mchingaji Mstaafu wa Kanisa la Kilutheri Tanzania (KKT), Richard Hananja
amesema Wazazi wana jukumu muhimu la kuwafundisha watoto maadili bora ili kuwasaidia kuwa watu wenye uhusiano mzuri na wengine na kuwa na tabia nzuri katika jamii.

“Watoto mara nyingi hutazama na kuiga vitendo vya wazazi wao. Hivyo, wazazi wanapaswa kuwa mfano mzuri wa maadili kama vile uaminifu, heshima, na upendo.
Ni muhimu wazazi wafundishe maadili kwa njia ya mazungumzo, lakini pia kwa vitendo. Kwa mfano, wakiwaonesha watoto jinsi ya kusaidiana na kushirikiana, watoto watajifunza kuwa na moyo wa kutoa.

Amesema thamani ya kazi ni bora kuliko mshahara hakuna mtu ambaye hakupita mikononi mwa mwalimu hivyo wanatumbua mchango wa wao katika Maadili.

“Shule ya sekondari ya Christon sio shule tu ni chuo cha maadili ni muhimu kuelewa nini maana ya maadili kizazi cha leo wazazi hawana habari ya Mungu na watoto hawana ya kwenda kwenye nyumba za ibada wakati ni muhimili wa maadili.

“Bado mnahitaji wazazi na watoto ongoeni na wazazi wenu kuhusu mambo mbalimbali na mfanye mambo yanaendana na maadili ya kitanzania,” amesema.

Ameongeza kuwa wanafunzi waliofanya mahafali leo wanapaswa kusoma elimu ni ya msingi na inawahitaji wajiepushe na makundi ya hovyo kujiingiza kwenye madawa ya kulevya yana haribu maisha yao na kutumia dawa za kulevya sio ujanja.

Amesisitiza kuwa wajiepushe na mpenzi ya jinsia moja, dawa za kulevya kwani vijana ni nguvu kazi wa Taifa la kesho na wazazi wanapaswa kuwasimamia watatoa wao na kuwafundisha maadili ya jaamii zetu za kitanzania.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule Sekondari ya.Wavulana Chriton, Augustine Minja amesema shule hiyo ilanza mwaka 2015 ikiwa na wanafunzi 86 hadi kufikia sasa kuna wanafunzi 615

Ameeleza kuwa maono ya shule hiyo ni kuwa walimu wakufundisha shule zingine kuwa nini wanafanya kuhakikisha wanafunzi wanafaulu vizuri katika mitahani yao ya mwishoo.

Amesema baadhi ya wazazi hawataki watoto wao kufanya kazi za mikono hiyi ni chagamoto hawatesi ila wanawatengenezea kuwa baba bora baadae.





Related Posts