Zidane aitaja janja ya Job

MSHAMBULIAJI chipukizi wa Azam, Zidane Sereri amesema kama kuna beki anayemuumiza akili inapotokea wanakutana katika mechi basi ni Dickson Job wa Yanga kwa aina ya ukabaji wake, unakuwa unahitaji akili kubwa kuvuka eneo lake.

Zidane ndiye aliyeinyima Simba pointi tatu baada ya kufunga bao la kusawazisha dakika mbili kabla ya mchezo kumalizika kwa sare mabao 2-2, alisema amekuwa akiwatazama mabeki mbalimbali wa Ligi Kuu ila anayemkubali zaidi  ni Job.

Alisema Job anatumia akili kubwa kudhibiti mashambulizi, kuliko nguvu jambo linalomuepusha kucheza rafu na kupata kadi ambazo hazina ulazima wa kuiumiza timu yake.

“Ni mara chache kumuona Job anapata kadi za hovyo hovyo anafanya kazi yake kwa umakini wa hali ya juu, beki kama huyo inahitaji kufikilia zaidi ili kupita eneo lake kwenda kufunga,” alisema Zidane mwenye mabao matano katika Ligi Kuu na kuongeza;

Nje na Job alisema anamkubali Idd Seleman ‘Nado’ ni mchezaji anayejituma na kuheshimu kazi yake na anamuona ni mfano wa kuigwa na wengine katika kikosi cha Azam.

Sereri alitua Azam kupitia dirisha dogo akitokea Dodoma Jiji na tangu ae na timu hiyo tayari ameifungia mabao mawili dhidi ya Mashujaa na Simba, huku mabao matatu akitoka nayo Dodoma Jiji.

Related Posts