Mlionunua tiketi za Dabi ujumbe wenu huu hapa

WAKATI mchezo wa Kariakoo Dabi ukiahirishwa, huku mashabiki wakiwa tayari wamekata tiketi swali lililopo ni watarudishiwa fedha zao au ndiyo wamepata hasara?

Kufuatia maswali kuwa mengi nini kitafanyika, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe ametoa ujumbe uwafikie wale wote waliokata tiketi mapema akisema mfumo wa ununuaji ulisitishwa mchana, lakini wahusika wala wasiwe na hofu.

“Mfumo wa ununuaji tiketi ulisitishwa saa 7 mchana ambapo hadi muda huo zilinunuliwa tiketi 40,000, ” amesema Kamwe.

“Wale waliokata tiketi wasiwe na wasiwasi tunasubiri kuona nini kitaamuliwa kwani utaratibu maalumu utafanyika kisha itatolewa taarifa rasmi.”

Tiketi za mchezo huo zilikuwa zikiuzwa Sh50,000 (Jukwaa la VIP A), Sh30,000 (Jukwaa la VIP B), Sh20,000 (Jukwaa la VIP C), 10,000 (Jukwa la Orange) na Sh5,000 (Jukwaa la Mzunguko) wakati Royal tiketi ni Sh150,000.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara ambao Yanga walikuwa wenyeji wa Simba uliopangwa kuchezwa leo Machi 8, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuanzia saa 1:15 usiku umeahirishwa na Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) kufuatia uamuzi wa Simba kugomea kucheza kidai imenyimwa haki ya kikanuni ya kufanya mazoezi kwenye uwanja wa mechi siku moja kabla.

Related Posts