NBAA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KIMATAIFA

 

Katika kuadhimisha siku ya Wanawake Kimataifa, wanawake wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wameshiriki maadhimisho hayo yaliyofanyika Machi 08, 2025 na kuadhimishwa jijini Dar es salaam katika Viwanja vya Leaders ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji.”

Siku ya Wanawake Kimataifa ilianzishwa kufuatia jitihada za wanawake 15,000 mwaka 1908 walipoandamana mjini New York Marekani wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi, ujira wa kuridhisha na haki ya kupiga kura. Kilikuwa ni chama cha kisoshalisti cha Amerika kilichotangaza kuwa ni siku ya kwanza ya kitaifa ya wanawake, mwaka mmoja baadaye. Wazo la kuwa siku ya kimataifa lilianzishwa na mwanamke kwa jina la Clara Zetkin. Yeye alipendekeza wazo hilo mwaka 1910 katika mkutano wa kimataifa wa wafanyakazi wanawake huko Copenhagen Denmark.

Picha mbalimbali za matukio ya wafanyakazi wanawake wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika maadhimisho ya Siku ya wanawake Kimataifa yaliyofanyika Machi 08, 2025 katika Viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila pamoja na viongozi mbalimbali wakiwapungia mikono wafanyakazi wanawake wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika maadhimisho ya Siku ya wanawake Kimataifa.

Related Posts