NYEPESI NYEPESI ZA DABI: Yanga, Simba hadi Pan na Red Stars

NDIVYO ukweli ulivyo. Yanga ina kila sababu ya kujiita Baba Lao katika soka la Tanzania, kwani unaambiwa, licha ya kusumbuana kwa sasa na Simba katika ubingwa wa Ligi Kuu, lakini klabu hiyo ndio iliyosababishwa kuzaliwa kwa Wekundu wa Msimbazi baada ya kujitenga kutoka Yanga mwaka 1936.

Kitu cha ajabu ni, Yanga ilikuwa na mgogoro mwingine mwaka 1975 na kusababisha kuzaliwa kwa klabu ya Pan Africans, wakati Simba nayo mwaka huo huo ilikumbwa na mgogoro uliozaa Nyota Nyekundu (Red Stars) moja ya timu zilizowahi kusumbua Ligi ya Tanzania kabla ya kupotea.

Hii ina maana kama Yanga isingezaliwa 1935, huenda hata Simba iliyojiengua isingekuwepo na hizo Pan na Nyota Nyekundu nazo zisingezaliwa na pengine hata leo hii tusingejadili Dabi ya Kariakoo!

Related Posts