Aziz KI, Nouma watemwa Burkina Faso

KIUNGO mshambuliaji nyota wa Yanga, Stephane Aziz Ki na beki wa kushoto wa Simba, Valentino Nouma wametemwa katika kikosi cha Burkina Faso kilichotangazwa kuitwa leo Jumatatu na kocha Brama Traore kwa ajili ya michezo miwili ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2026

Burkina Faso itakuwa nyumbani Machi 16 2025 kucheza mchezo wa tano wa makundi dhidi ya Djibouti kabla ya kusafiri kuifuata Guinea Bissau  Machi 23.

Ikumbukwe kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 alikuwepo katika kikosi kilichocheza mechi za mwanzoni za michuano hiyo akicheza michezo mitatu na kutoa pasi iliyozaa bao.

Burkina Faso inashika nafasi ya tatu katika Kundi A ikivuna pointi tano katika michezo minne iliyocheza, nyuma ya Guinea Bissau yenye alama 6 na Misri inayoongoza kundi hilo ikiwa na pointi 10.

Kikosi kamili cha Burkina Faso kilichoitwa leo ni;

Makipa ni Kylian Nikiema, Hervé Koffi, Farid Ouédraogo, Mabeki wakiwa ni; Issa Kabore, Steeve Yago, Edmond Tapsoba, Nasser Djiga Issoufou Dayo, Adamo Nagalo,Kouassi Guy Arsène na Mohamed Yabre.

Viungo ni; Memel Dao, Cedric Badolo Mohamed Zoungrana, Blati Toure Josue Tiendrebeogo, Saidou Simpore, Dramane Salou, Ishmaila Ouédraogo wakati washambuliaji wakiwa ni; Franck Lassina Traore Dango Ouattara, Bertrand Traore, Hassane Bande, Mohamed Konate na Cyriaque Iri.

Related Posts