Simba Queens yataka rekodi tatu bongo

KOCHA wa Simba Queens, Yussif Basigi amesema anatamani kuandika rekodi tatu kwenye ligi ya Tanzania ambayo ndio msimu wake wa kwanza kuitumikia.

Kocha huyo alijiunga na Simba akitokea Hasacaas Ladies ya Ghana na ukiwa msimu wake wa kwanza kwenye Ligi hajapoteza mchezo wowote akitoa sare moja na JKT Queens na ushindi mechi 11.

Akizungumza na Mwanaspoti, Basigi alisema rekodi ya kwanza anatamani kuchukua ubingwa wa Tanzania na kuandika historia akiwa nje ya Ghana, pili kutopoteza mchezo wowote na tatu kuipeleka timu hiyo michuano ya kimataifa.

Aliongeza kuwa hayo anatamani kuyafanya kama kocha kufikia malengo ya klabu ambayo inapambana kutetea ubingwa wake.

“Ligi ya Tanzania ni ngumu tofuati na Ghana na huku watu wako siriazi na timu zao naona hata mashabiki wanakuja uwanjani ni jambo kubwa kuwapa hamasa wachezaji,” alisema Basigi na kuongeza:

“Natamani kuweka rekodi hizo kama kocha inakuandikia CV nzuri hasa kushiriki mashindano ya kimataifa ambayo kama tutakuwa mabingwa tutakuwa moja ya timu hizo.”

Related Posts