Profesa Assad, Mhadhiri UDSM wawapiga darasa vigogo Chadema

Dar es Salaam. Viongozi mbalimbali wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakiwemo wajumbe wa kamati kuu watajifungia kwa siku mbili kupigwa darasa la uongozi.

Mafunzo hayo kwa viongozi akiwemo Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu yameanza leo Jumatano, Machi 12, 2025 makao makuu ya chama hicho, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Walengwa wa mafunzo hayo ni wajumbe wa kamati kuu, sekretarieti ya kamati kuu, makatibu wa Kanda na viongozi wengine yanatolewa kipindi ambacho kuna mabadiliko ya viongozi hao.

Mabadiliko hayo yanatokana na kuhitimishwa kwa chaguzi za chama hicho Januari 21, 2025 kwa kupatikana kwa viongozi wapya akiwemo Lissu ambaye alimshinda Freeman Mbowe. Aidha, Makamu wenyeviti na naibu makatibu wakuu nao ni wapya isipokuwa Katibu Mkuu, John Mnyika.

Makatibu wa kanda kati ya 10 wa chama hicho, watano ni wapya sawa na wajumbe wa sekretarieti ambao wameteuliwa jana Jumanne, Machi 11, 2025 na kamati kuu.

Katika siku ya kwanza ya mafunzo hayo, watoa mada walikuwa watatu ambao ni aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wa zamani, Profesa Mussa Assad na  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Philbert Komu.

Kesho Alhamisi, itakuwa siku ya mwisho ya mafunzo hayo na kutakuwa na watoa mada wengine.

Related Posts