Baraza la vyama vya siasa nchini limekemea vikali kitendo cha Chama cha ACT WAZALENDO kuchapisha na kusambanza kipeperushi kinachobeza kazi zinazofanywa na baraza hilo huku kikisusia kushiriki kikao kilichoketi machi 12 na 13 mkoani Morogoro.
Hayo yameelezwa na wajumbe wa baraza hilo wakati wa kikao cha kawaida cha baraza la vyama vya siasa kilichoketi kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu vyama hivyo hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu mkuu wa chama cha National League For Democracy (NLD) Doyo Hassan Doyo amesema kuwa baraza hilo ni chombo kilichundwa kishereia kupitia bunge la jamuhuri ya muungano wa tanzania hivyo mtu au chama chochote kinaachosimama na kudharau kazi za baraza lazima tumkemee kwa nguvu zote.
“juzi tumeona statimenti iliyotolewa na chama cha ACT WAZALENDO kuwa hawatashiriki baraza la vyama vya siasa kwasababu kuwa baraza halifanyi kazi stahiki kwa ajili ya kuvisaidia vyama na kutunza demokrasia nchini, kitu ambacho sisi kama wajumbe wa baraza hili tunaona sio sawa” alimesema Doyo
Miaka mitano iliyopita vyama vya sisa vilizuiliwa kufanya mikutana ya hadhara lakini kupitia kazi za baraza hili tumeshuhudia baada ya kikosi kazi cha baraza kuunda sasa vyama vya siasa vinafanya mikutano kwa uhuru ameongeza.
Hata hivyo amesema kuwa chama cha ACT Wazalendo ni miongoni mwa vyama vilivyosaidiwa sana na baraza hilo katika kufikia malengo yake tangu kilipo anzishwa hivyo hakikuwa na sababu ya kubeza kazi za baraza.
Kwa upande wake katibu mkuu wa chama cha democratic party DP ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya siasa na bunge Abdul Mluya amesema kuwa baraza limekuwa kiunganishi kikubwa kati ya vyama vya siasa na saerikali katika masuala mbalimbali yanayohusu vyama hivyo mara kwa mara.
“Ukiona watu wanatusi chombo ambacho hata kiongozi wao mkuu ndicho kilichompa heshima, halafu unaandika kipeperushi ambacho hakina lugha ya staha bali ni lugha ya kifedhuli watanzania muwasamehe hawa chama chao bado ni kichanga wanatafuta kiki ya kutokea ili wananchi wajue kuwa nao wapo”. Amesema
Aidha ameeleza kuwa kwa kitendo cha chama cha ACT Wazalendo kuchapisha ujumba unaolenga kunajisi chombo kilichoundwa kisheria sio jambo la kufumbia macho na hawapaswi kulaumiwa kwa kuwa ni chama kichanga mno ukilinganisha na vyama vingine.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari wakati juu ya maazimio ya baraza la vyama vya siasa mwenyekiti wa baraza hilo Juma Ally Khatibu amesema kuwa baraza halitawavumilia wanasiasa watakao tumia majukwaa hayo kuhamasisha vurugu na uvunjifu wa amani ya watanzania.
Mwenyekiti amesema kuwa wakati taifa likielekea kufanya uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwezi oktoba mwaka huu baraza halite fumbia macho wanasiasa watakao hamasisha wananchi kukiuka misingi ya katiba na kukiuka maadili ya kitanzania.
Hatahivyo baraza hilo limevihasa vyama vyote vya siasa nchini kuheshimu katiba, sharia za nchi pamoja na kuheshimu maadili ya uchaguzi sambamba na kudumisha amani na utulivu ulipo.