KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA SERIKALI KWA MABORESHO MAKUBWA YA MIUNDOMBINU BANDARI YA TANGA


Na Oscar Assenga,TANGA

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeipongeza Serikali kwa maboresho makubwa ya miundombinu katika Bandari ya Tanga ambayo yamekuwa chachu ya kuongeza ufanisi katika utendaji wake.

Kauli ya Kamati hiyo ilitolewa leo na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Seleman Moshi Kakoso baada ya kumaliza ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maboresho na miundombinu ya sekta ya Uchukuzi katika Mkoa wa Tanga.

Alisema kwamba kamati hiyo imeridhishwa na utendaji kazi wa mamlaka hiyo hasa baada ya maboresho ya miundombinu iliyofanywa na Serikali na hivyo kuiongezea ufanisi wa kazi pamoja na ukusanyaji wa mapato.

“Kwa kweli sisi kama Kamati tumeridhishwa na utendaji kazi wa mamlaka ya Bandari na nieleze kwamba tutaendelea kuisadia TPA kutimiza maono ya Rais na kufikia malengo yao na Serikali kwa ujumla”Alisema

Awali akizungumza Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile aliishukuru kamati kwa ziara yao iliyowawezesha kujionea kazi kubwa inayofanywa na Serikali katika katika kuboresha sekta hiyo.

“Niwahakikishie kamati kwamba maoni, ushauri na maelekezo mliyoyatoa yatafanyiwa kazi kuhakikisha mkoa wa Tanga unafunguka kiuchumi kutokana na maboresho yanayoendelea kufanywa na Wizara ya Uchukuzi”Alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) Plasduce Mbosa alisema kukamilika awamu ya mbili za maboresho ya maboresho ya Bandari ya Tanga kwa gharama ya shilingi Bilioni 429.1 kumekuwa chachu ya maendeleo na kufungua ushoroba wa kanda ya kaskazini.

“Niishukuru kamati ya kudumu ya Bunge Miundombinu kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa TPA ili mamlaka hiyo iweze kutekeleza mipango yake ya maboresho ya Bandari na kuwa chachu ya maendeleo ya uchumi wa Taifa “Alisema

Related Posts