NA DENIS MLOWE, IRINGA
KAMATI ya Ulinzi na Usalama Barabarani mkoa wa Iringa imekabidhi gari la kisasa kwa jeshi la polisi mkoa wa Iringa kwa ajili ya kuimarisha doria za usalama barabarani.
Akizungumza wakati wa kukabidhi gari hilo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Salim Abri (Asas) alisema kuwa gari hilo limetolewa na kamati hiyo baada ya kuongezeka kwa changamoto mbalimbali za barabarani hivyo gari hilo la kisasa litasaidia katika kuimarisha doria kwa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kazi nyingine za jeshi hilo.
Aliongeza kuwa gari hilo litaongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao kwani kamati inatambua mchango mkubwa wa Jeshi la katika ulinzi na usalama wa raia hasa katika masuala ya barabarani ambapo kumekuwa na ongezeko la vyombo vya moto na changamoto kuongezeka.
Alissema kuwa kama kamati ya usalama barabarani waliona kwamba jeshi la Polisi linahitaji vitendea kazi ikiwemo gari hivyo lengo ni kuongeza usimamizi wa umakini unahitajika kwani inatakuwa vigumu kwa jeshi kufatilia kama hakuna vitenda kazi.
Akipokea msaada huo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi licha ya kushukuru msaada huo alisema kuwa gari hilo litatumika ya kama inavyostahili na kuongeza kuwa wao kama jeshi linauheshimu msaada huo kutoka kamati ya ulinzi na Usalama Barabarani chini Salim Abri Asas.
Alisema kuwa gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser Deluxe limenunuliwa kwa sh milioni 100 kutokana na ada za ukaguzi na mchango kutoka kwa mwenyekiti wa usalama barabarani Salim Abri aliyechangia kwa kiasi kikubwa.
SACP Bukumbi alisema kuwa jeshi hilo limekuwa likikusanya ada za ukaguzi ambazo fedha hizo upelekwa makao makuu na makusanyo hayo ya mkoa hurudishwa nusu kwa kamati na kisha hutumika kwa kazi mbalimbali hivyo kutokana na kamati hiyo kuamua kutumia fedha hizo kwa ajili ya ununuzi wa gari hilo la kisasa.
Aliongeza kuwa katika kuimarisha usalama jeshi la Polisi mkoa wa Iringa limewapeleka mafunzo wakaguzi na askari 90 kwa ajili ya kujifunza udereva Veta ili kuwa na askari na wakaguzi wenye weledi kwenye kazi .
Aidha alisema wao kama taasisi muhimu ya Serikali wanawakaribisha wote wenye malengo ya kutoka misaada mbalimbali itayolisaidia Jeshi hilo kuzidi kuongeza ufanisi huku akisisitiza kuwa milango ipo wazi kwa wote wenye nia hiyo kama walivyofanya kampuni ya Vidam ambao wamtoa msaada wa pikipiki kwa jeshi hilo.
Naye Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya Usalam Barabarani, Glory Mtui alisema kuwa gari hilo litasaidia kwa kiasi kikubwa kwa kikosi cha usalama barabarani katika kufanya dolia za masafa mafupi na marefu na kutumika kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii inayotumia vyombo vya moto mkoani hapa.
Alisema kuwa ubora wa gari hilo licha ya kufanya doria litawezesha shughuli za ulinzi na usalama katika mkoa wa Iringa kufanyika kwa ufanisi zaidi.