Majina walimu wapya walioajiriwa serikalini haya hapa

Dar es Salaam. Serikali imewaita kazini walimu wapya 319 wa fani mbalimbali ambapo halmashauri saba zimenufaika na ingizo hilo jipya la walimu.

Taarifa ya kuitwa kazini kwa walimu hao imetolewa jana Machi 12, 2025 na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

“Katibu wa Sekretarieti ya Ajira anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya Septemba 4, 2024 na Februari 24, 2025 kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili.

“Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana,”imeeleza taarifa hiyo.

Walimu hao wamepangiwa kazi katika maeneo yafuatayo: Halmashauri ya Manispaa ya Songea, Halmashauri ya Manispaa ya Kahama,  Halmashauri ya Jiji la Arusha, Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Halmashauri ya Wilaya ya Magu na Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua.

Related Posts