Na. Mwandishi Jeshi la Polisi Arusha.
Jeshi la Polisi Mkoa watu Arusha limesema kuwa tarehe 13, machi,2025 muda wa saa 12:30 asubuhi huko katika maeneo ya mtaa wa njiro ndogo kata ya sokoni one katika halimashauri ya jiji la Arusha watu wawili wasiofahamika majina wanaume wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 28 walifariki dunia baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao na watu wasiofahamika huku likawaonya watu wanajichukulia sheria Mkononi.
Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisii (SACP) Justine Masejo amesema kuwa Watu hao walishambuliwa mara baada ya kuiba pikipiki iliyokuwa imeegeshwa Jirani na kituo cha mafuta cha simba oil kilichopo eneo la njiro ndogo ambapo pia walichoma pikipiki yenye namba ya usajili Mc 438 ESG aina ya Sinoray iliyokuwa inatumiwa na watu hao.
Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi Mkoani humo linaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hili ili kuibaini chanzo cha tukio na hatua zitachukuliwa kwa wale watakaobainika kuhusika na tukio hili.
SACP Masejo amebainisha kuwa miili ya marehemu imehifadhiwa katika kituo cha Afya Murieti kwa ajili ya utambuzi na uchunguzi wa daktari.
Kamanda Masejo Pia amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawaonya watu wanaoendelea kujichukulia sheria mkononi kuwa waache mara moja na badala yake watoe taarifa za uhalifu na wahalifu ili hatua sstahiki ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria.