Songamnara, Kilwa kisiwani kinara kuvutia watalii

Kilwa. Mamlaka ya wanyamapori Tanzania (Tawa) imeyataja maeneo ya Songamnara na Kilwa kisiwani kuwa kinara kwa kutembelewa na watalii mkoani Lindi.

Hayo yamesemwa Machi 12, 2025 na Kamishna Msaidizi wa uhifadhi Kanda ya Kusini Mashariki, Hadija Malongo akizungumza wakati wa kuwapokea watalii katika eneo la Songamnara.

Hadija amesema kuwa hadi sasa Tawa wameshapokea watalii zaidi ya 1,000 ambao wamekuja kipindi cha Januari hadi Machi 2025.

“Tunawashukuru wadau wa sekta ya utalii ambapo kwa sasa katika maeneo ya Songamnara na Kilwa kisiwani yanaongoza kutembelewa na watalii, wadau hao ikiwemo Kampuni ya Abercrombie & Kent Tours Ltd imeweza kuongeza watalii.

“Serikali inataka ifikapo 2025 /2026 tuwe tumeshaingiza watalii milioni 5, kiukweli tunamshukuru Mungu jitihada za kuongeza watalii zinafanyika na zinaonekana, Serikali imeweka kiasi cha zaidi ya Sh2 bilioni kuboresha miundombinu ya maeneo wanayofikia watalii,”amesema na kuongeza Hadija

Kaimu Msaidizi wa uhifadhi wa wanayamapori, Saidi Mshana amesema watalii hao wanasaidia kuongeza kipato cha Wilaya ya Kilwa na Taifa kwa ujumla.

Mohamed Salim, ambaye ni mjasiriamali kutoka Kilwa ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha kwa ajili ya ukarabati uliyofanywa na Tawa ili kuvutia watalii wengi.

Related Posts