BENCHI la Ufundi la Yanga limetoa siku Sita za mapumziko kwa wachezaji wake baadhi Stephen Aziz Kin a Pacome Zouzoua baada ya mchezo wa jana dhidi ya Coastal Union ya Mkoani Tanga ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Chanzo cha Habari kutoka ndani ya Benchi la Ufundi la Yanga, kikosi hicho kinatarajiwa kurejea mazoezini Jumatano ijayo ambayo Marchi 19, mwaka huu.
Chanzo hicho kilisema kuwa kikosi hicho kitarejea kambini kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara watakaocheza dhidi ya Tabora United Aprili 01, mwaka huu Mkoani Tabora.