Jiandae na mabadiliko haya unapofunga

Hivi sasa Wakristo na Waislamu, wapo katika mfungo, hujinyima kula kwa saa kadhaa ili kutimiza imani zao.

Bahati mbaya si wote wanaofunga miili yao huwa na ustahimilivu wa kushinda bila kula, hivyo hupata matatizo ya kiafya.

Ikiwa umezoea kupata kifungua kinywa, chakula cha mchana, chakula cha jioni na vitafunio vya katikati kabla ya mlo mkuu, wakati wa kufunga kunaweza kuwa na changamoto kadhaa za kiafya.

Ni kawaida kupata dalili za mapema zifuatazo wakati wa kufunga na kushinda bila kula kwa muda mrefu.

Ingawa si tishio kuweza kusababisha kifo au madhara makubwa. Ndio maana hakuna matukio mengi ya watu kupoteza maisha wakati wa kufunga.

Ni kawaida watu kuhisi njaa kali katika vipindi vyao vya kufunga, na huambatana na tumbo kuuma na kuunguruma.

Utafiti mdogo sana umelinganisha njaa ya muda mrefu kwa watu walio na ratiba tofauti za kufunga mara kwa mara. Kwa ujumla, unaweza kutarajia kuwa na njaa zaidi kuliko kawaida mwanzoni mwa mfungo.

Baadhi ya tafiti zinaripoti kuwa hali hii huisha kwa kadiri siku za kufunga zinavyoenda, lakini sivyo hivyo kila wakati. Mingurumo ya tumbo hutokana na tumbo kuwa tupu na uchokozi wa juisi na titindali za tumboni.

Wakati wa mfungo, huenda ukawa na uwezekano mkubwa wa kuumwa na kichwa. Hatari hii ni ya juu kwa watu ambao hufunga kwa zaidi ya saa 16 kwa siku.

Maumivu ya kichwa huwa ya wastani hadi ya juu, sababu kubwa huwa ni upungufu wa maji mwili na chumvi chumvi.

Uchovu na mabadiliko ya hisia

Ni kawaida kupata hali ya uchovu wakati wa kufunga hii ni kutokana na upungufu wa maji mwilini na kukosa lishe ambayo ndio chanzo cha nguvu mwilini.

Na pia ni kawaida kubadilika hisia kutokana na hali ya maumivu ya kichwa au tumbo na hisia za njaa kali.

Zipo tafiti zinapendekeza kuwa kufunga mara kwa mara kunaweza kuboresha hisia na uchovu.

Ni muhimu kuzingatia mwili wako unavyokuwa wakati wa kufunga.

Unapofunga, unapoteza chumvi na maji kwenye haja zote, jasho, kupumua na kuongea. Hali hii huwa katika siku 2-4 za kwanza.

Baadhi ya dalili za mapema ni kizunguzungu, uchovu na maumivu ya kichwa na kukosa utulivu, kukosa umakini na maamuzi dhaifu na kuyumba kihisia.

Kufunga mara kwa mara kunaweza kusababisha shida za kulala.

Hii ni kwa sababu nyakati zako mpya za mlo huingilia mchakato wa usingizi katika ubongo ujulikanao kwa jina la mitetemo ya ‘circadian’.

Kwa hiyo, ikiwa una matatizo ya usingizi kuna uwezekano mwili wako unarekebisha ratiba mpya, na hapo baadaye huboreka na kuisha.

Kufunga kwa muda mrefu kunaweza kuongeza hatari yako ya kupoteza virutubisho vingi mwilini.

Dalili za utapiamlo ni pamoja kupoteza uzito bila kukusudia, kuhisi baridi isivyo kawaida, uchovu au udhaifu, magonjwa ya mara kwa mara, kukosa utulivu, ngozi na nywele kupoteza nuru, kukosa utulivu na mabadiliko ya hisia.

Habari nzuri ni kwamba si kila mfungaji hupata dalili hizi, kwa sababu mwili unajitengenezea ustahimilivu kukabiliana na hali ngumu ya kushinda bila kula kwa muda mrefu. Ndio maana wafungaji wengi huwa iimara kiafya.

Kitabibu inashauriwa wajawazito, watoto, wazee sana na wenye magonjwa mbalimbali, kutokufunga kwani miili yao inahitajj kuwa imara zaidi kiafya.

Usikose wiki ijayo njia za kukabiliana na hali hizi na baadhi ya matatizo ya kiafya yanayotokea baada ya kufuturu.

Related Posts