PAC YARIDHISHWA NA UJENZI WA GHALA JIPYA MSD DODOMA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Naghenjwa Kaboyoka imetembelea  na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa ghala la kisasa la kuhifadhia bidhaa za afya linalojengwa na Bohari ya Dawa (MSD) katika eneo la Kizota, Mkoani Dodoma.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Kaboyoka ameipongeza MSD kwa kazi kubwa inayoifanya ya ujenzi wa ghala kubwa la kisasa ambalo litakwenda kutatua changamoto za utunzaji wa bidhaa za afya kwa kiasi kikubwa.  “Kazi mnayoifanya inaonekana, leo tumeona uwekezaji mkubwa wa ghala hili kubwa na la Kisasa ambalo lina Ubora wa kimataifa, serikali imewekeza hapa zaidi ya Bilioni 23.7 kujenga ghala hili lenye mita za mraba 7,200 sisi kama kamati tunategemea kuona changamoto za utunzaji wa bidhaa za afya zinapungua”.

Aidha, pamoja na kupongeza ujenzi wa maghala Mhe. Kaboyoka amepongeza namna MSD inavyosambaza mashine za kusafisha damu kwa wagonjwa wa Figo ambazo zimepelekea kupunguza ghalama za huduma hiyo kwa wananchi. “Siku hizi magonjwa ya figo yamekuwa mengi hadi watoto wadogo wanapata ugonjwa huo tunaishukuru MSD kwa kupunguza gharama ya huduma hii baada ya MSD kuanza kusambaza mashine za kusafisha damu sasa hivi tunaona huduma hiyo imepungua gharama kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya MSD Bi. Rosemary Silaa amesema MSD itaendelea na ujenzi wa Maghala mapya kwa lengo la kutatua changamoto za utunzaji wa bidhaa za afya ambapo baada ya ujenzi huu wa Dodoma na Mtwara MSD itaanza ujenzi wa maghala mapya mkoani Chato, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Mwanza na Ruvuma.   MSD kwasasa inauwezo wa kutunza bidhaa hizo kwenye mita za mraba 56,000 huku MSD ikiwa na uhitaji wa mita za mraba 100,000 kukidhi mahitaji yake ya utunzaji.

 

Related Posts