Mambo yanaonekana kutokuwa mazuri kwa timu 10 ambazo bado hazina pointi za kuzifanya ziwe katika uwezekano salama wa kubakia katika Ligi Kuu ingawa timu sita zilizopo juu kwenye msimamo wa ligi hazina presha kubwa.
Zimebaki raundi saba tu msimu kumalizika na timu hizo 10 kila moja hivi sasa hapana shaka inajipanga na kufanya tathmini ya jinsi gani inavyoweza kucha karata katika mechi zake saba zilizobakia ili iweze kunusurika na janga la kushuka daraja.
Ifuatayo ni orodha ya timu 10 zilizo katika mdomo wa mamba kwenye Ligi Kuu na tathmini ya mtego ambao kila moja inakabiliana nayo kwa raundi zilizobakia.
COASTAL UNION – Pointi 25
TANZANIA PRISONS – Pointi 18