Na Pamela Mollel,Arusha
Serikali kupitia Wizara ya mambo ya ndani imewahakikishia wawekezaji pamoja na watanzania kuwa Tanzania ipo salama na inafursa nyingi ukilinganisha na Nchi zingine Duniani
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Innocent Bashungwa mara baada ya kufungua Mkutano wa 62 wa bodi ya kimataifa ya uwazi na uwajibikaji (EITI)
Waziri Bashungwa anasema kwa kuwepo na Amani na Mshikamano ndani ya Nchi inasaidia mazingira wezeshi kwa wawekezaji
“Waandishi wa habari mnajukumu la kutangaza Nchi yetu kwa mambo mazuri yaliyopo ikiwemo Amani na Mshikamano,bila Amani huwezi kufanya lolote “Waziri Bashungwa
Ameongeza kuwa kupitia uongozi Mahari wa Rais wa nchi Mh Samia Suluhu Hassan Tanzania sasahivi inapata mikutano mikubwa ya kimataifa ni kutokana na Amani iliyopo.
Aidha aliwataka waandishi wa habari kuendelea kuelimisha umma juu ya kazi nzuri inayofanywa na serikali kupitia EITI kwa kushirikiana na kampuni zilizopo katika sekta ya madini,gesi,mafuta pamoja na Asasi zisizokuwa za kiraia
“Niombe Sekretarieti itenge programu ya mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu EITI ili waweze kutoa taarifaa sahihi kwa umma”anasisitiza Bashungwa
Naye Waziri wa madini Anthony Mavunde anasema Tanzania inasomeka vizuri kwenye ramani,ya dunia kutokana na kazi kubwa inayofanywa na Rais Samia ya kuboresha mahusiano
Ameongeza kuwa kupitia mkutano wa kimataifa wa uwazi na uwajibikaji Duniani ni heshima kubwa kwa nchi kuwa mwenyeji wa mkutano huo.