Dar es Salam. Uyoga ni chanzo kizuri cha madini ya chuma, shaba na protini ambayo hufanya vizuri katika mwilini wa binadamu.
Kama ulikuwa hufahamu uyoga una nyuzi nyuzi nyingi na hauna mafuta na chumvi ya sodium.
Mtaalamu wa Sayansi na Teknolojia ya Chakula, Francis Modaha, anasema uyoga una kundi la vitamini B kwa wingi, yaani vitamini B2 (Riboflavin), Niacin na Pantothenic acid.
Anasema kundi hilo la vitamini B huusaidia mwili kupata nishati lishe kutokana na virutubishi vya protini, mafuta na wanga.
Modaha anasema mbali na kuwa na vitamini B, pia una una vitamini D, madini ya selenium ambayo husaidia kuimarisha kinga mwili na kuusaidia mwili kukabiliana na madhara yoyote na kupunguza kasi ya uharibifu wa viini vya mwili.
” Madini ya copper yaliyopo katija uyoga, husaidia kuzalisha nishati lishe, mifupa laini mwilini na seli nyekundu za damu ambayo hubeba hewa ya oxijeni katika sehemu zote za mwili” anasema Modaha.
Anabainisha kuwa uyoga husaidia kuimarisha mishipa ya fahamu.
Modaha ambaye alishawahi kuwa ofisa Mtafiti Mwandamizi wa Sayansi na Chakula, kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe( TFNC) anafafanua kuwa uyoga ni chanzo kizuri cha madini ya chuma, shaba na protini ambayo hufanya vizuri katika mwilini wa binadamu.
Anasema, madini ya potassium ambayo hudumisha kiwango kizuri cha shinikizo la damu, utendaji kazi mzuri wa moyo na misuli.
Anabainisha kuwa uyoga ni mzuri kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari kwa sababu inapunguza kisukari kwa watu wenye kisukari type two.
” Lakini uyoga una vitamini C pamoja na kiasi kidogo cha vitamini A, ambacho husaidia katika kupambana na matatizo mbalimbali yakiwemo yale ya msongo wa mawazo” anasema Modaha
Pia, uyoga ni mzuri pia kwa watu wanaosumbuliwa na msongo mawazo, lakini madini kama ya chuma hutengeneza damu mwilini.
Anafafanua kuwa uyoga ni mzuri pia kwa watu wanaosumbuliwa na msongo mawazo, lakini madini kama ya chuma hutengeneza damu mwilini.
“Watu wanaokula uyoga mara kwa mara hujiweka kwenye nafasi ya kuwa na hali nzuri hususani kwa wale matatizo ya msongo wa mawazo” anabainisha.
Lakini vitamini B iliyopo katika uyoga, ina uwezo wa kuzuia uchovu wa mwili na akili hasa wakati wa kazi nyingi, huku Vitamin B3 husaidia kupunguza kiwango cha lehemu mwilini, wakati Vitamini B6 huondoa hatari ya mtu kupatwa na shambulio la moyo.
” Uyoga ni mzuri kwa afya ya moyo, lakini huongeza uelewa na hutunza kumbukumbu, pia unasaidia misuli kufanya kazi vizuri” anaongeza.
Hata hivyo, anashauri watu wapendelee kula uyoga mara kwa mara kwa ajili ya kulinda afya zao.