Benki ya Exim Yaandaa Futari Tanga na Zanzibar Kuimarisha Uhusiano wa Kijamii

Benki ya Exim Tanzania imeandaa futari maalum Tanga na Zanzibar, ikikusanya pamoja wateja wake, viongozi wa dini, na wadau wakuu kwa jioni ya shukrani, mshikamano, na tafakari katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan. Hafla hizi zilitoa fursa ya kusherehekea maadili ya ukarimu, uadilifu, na msaada wa kijamii—ambayo yanawiana na misingi ya Uislamu pamoja na dhamira ya Benki ya Exim ya kuwawezesha watu kifedha na kuwajibika kwa jamii.

Hafla hizi za futari ni sehemu ya dhamira pana ya Benki ya Exim ya kushirikiana na wateja wake na kusaidia jamii kupitia miradi mbalimbali ya kijamii. Mbali na kutoa huduma za kifedha zinazozingatia misingi ya sheria, benki hiyo inaendelea kuwekeza katika programu zinazolenga kuinua biashara na watu binafsi huku ikikuza maadili ya kibenki yenye uwazi na uadilifu.

Benki ya Exim inaendelea kuwa mshirika wa kuaminika wa kifedha, ikihakikisha kuwa huduma zake si tu zinakidhi mahitaji ya wateja wake, bali pia zinachangia ustawi wa jamii kwa ujumla.

Sheikh Mkuu wa Mkoa Wa Tanga, Sheikh Juma Luwuchu (kulia), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Bw Jaffari Matundu (kati) na Mkuu wa Kitengo cha Hazina na Masoko ya Dunia wa benki ya Exim, Nelson Kishanda wakifuturu pamoja wakati wa hafla ya mfungo wa mwezi wa Ramadhan kama sehemu ya kuoneshaa umoja, mshikamano na upendo katika tukio lililofanyika mnamo tarehe 13 Machi 2025 mkoani Tanga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Mheshimiwa Ali Suleiman Ameir akipakuwa chakula wakati wa hafla ya Iftar na viongozi, waumini wa dini ya Kiislamu na wateja wa Benki ya Exim wakati wa kupata futari iliyoandaliwa na benki hiyo kama sehemu ya shukrani, mshikamano, na umoja katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Verde Zanzibar mnamo tarehe 13 Machi 2025.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Mheshimiwa Ali Suleiman Ameir, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi, akizungumza na viongozi wa dini, waumini wa dini ya Kiislamu na wateja wa Benki ya Exim wakati wa futari iliyoandaliwa na benki hiyo kama sehemu ya shukrani, mshikamano, na umoja katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Verde Zanzibar mnamo tarehe 13 Machi 2025.

Related Posts