MABONDIA Karim Mandonga ‘Mtu Kazi’ na Said Mbelwa wanapeleka burudani ya ngumi mjini Ruangwa, Lindi.
Pambano la Light Heavy litachezwa siku ya Idd Pili na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Mapromota Tanzania, Everest Ernest alisema pambano hilo litaambatana na mapambano mengine 10 ya utangulizi yatakayojumuisha na mabondia kutoka Lindi.
Hilo litakuwa pambano la tatu kwa mabondia hao ambapo mawili yaliyopita moja Mandonga alishinda na la mwisho lilimalizika kwa sare.
Akijinadi kuhusu pambano hilo, Mandonga alisema amekuja na ngumi mpya aina ya Kaniki ambayo ndio ataitumia dhidi ya mpinzani wake.
Mbelwa alisema haamini kama Mandonga ni mtu kazi na hadi sasa bado hakubaliani na uamuzi wa pambano la mwisho walilokutana ambalo lilimalizika kwa sare.