Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Kuombea uchaguzi mkuu 2025 ndugu Alex Msama, anatarajia kufanya tamasha kubwa la kuombea uchaguzi nchi nzima,akianza na jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam,Mwandaaji wa tamasha hilo Ndugu Alex Msama, amesema tamasha hilo litafanyika tarehe 20, Aprili 2025 katika jiji la Dar es Salaam na baadae litasambaa katika mikoa mingine 26 ya Tanzania Bara.
“kwa ujumla Maandalizi ya tamasha hilo mpaka sasa yanaendelea vizuri,na tunawakaribisha Wadhamini mbalimbali kuja kutuunga mkono kufanikisha Tamasha hili kubwa ambalo maalum kuomba uchaguzi ufanyika kwa amani,upendo na utulivu”,amefafanua Ndugu Msama .
Amesema kwa sasa jambo kubwa linalofanyika ni kuendelea kuzungumza na wafadhili mbalimbali, na kwamba wakifanikiwa kupata Wadhamini, basi tamasha hilo litakuwa halina kingilio,Watu wote wataingia bule.
Akifafanua zaidi Msama amebainisha kuwa tamasha hilo lenye umuhimu mkubwa kwa nchi yetu,hasa kwa wakati huu tunaokwenda kwenye uchaguzi,litawakutanisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili ndani na nje ya nchi.