TUNASEMA SAMIA MITANO TENA KWASABABU ANAYOYAFANYA WOTE TUNAYAONA-WASIRA

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Songwe

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Stephen Wasira amesema wanaposema Rais Samia Suluhu Hassan MITANO TENA ni kwasababu anayofanya yanaonekana kwa Watanzania…

Wasira ameyasema hayo leo Machi 15,2025 wilayani Mbozi mkoani Songwe baada ya kukagua ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe na kushiriki ujenzi pamoja na ujenzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Kanda ambapo amesema Serikali imedhamiria kusogeza huduma karibu na wananchi.

“Serikali imeendelea kusogeza huduma karibu na wananchi ,kila Kijiji tunampango wa kuwa na Zahanati Kwahiyo unatoka nyumbani kwako unakwenda kwenye Zahanati ikishindikana unakwenda kilometa chache katika kituo cha afya..

“Ukishindikana unaenda Hospitali na ukishindikana unaenda Hospitali ya rufaa ,ni kama vile Mwananchi anavyoenda mahakama ya Mwanzo hadi Mahakama kuu .Hiyo ndio kazi inafanywa na Serikali ya CCM

“Nanahodha wa kazi hii ni Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, kwahiyo tunaposema Samia mitano tena hatusemi uongo bali kwa mambo ya kweli yanayotokea ,hatupigi maneno tu bali tunasema Samia mitano  kwasababu kuna kazi anafanya na zinaoneokana

“Lakini ninyi muje hapa na mdanganywe na maneno matupu ya watu wanapita mara waende Angola wafukuzwe mtapoteza wakati wenu.

 

 

Related Posts