Hotuba Nzito Ya Rais Mwinyi Kwenye Mashindano Ya Qu’raan Tukufu – Video – Global Publishers



Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi

Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Mashindano ya 25 ya Qur’an Tukufu, amesema mashindano hayo ni ishara ya amani na uhuru wa kuabudu uliopo nchini Tanzania.

Akizungumza katika mashindano hayo yaliyofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa leo Machi 16, 2025, Dar es Salaam, Rais Mwinyi amesema serikali ya Tanzania inatoa ushirikiano wa kutosha katika shughuli za kidini bila kujali dhehebu la mtu, jambo linalosaidia kudumisha umoja, amani, na utulivu nchini.

Amehimiza Waislamu kuisoma na kuihifadhi Qur’an Tukufu, hasa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, huku wakitubu na kusaidia wenye uhitaji.

Aidha, ameipongeza Taasisi ya Al-Hikma Foundation na wadhamini wake, wakiwemo Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ Bank), kwa kufanikisha mashindano haya ya kimataifa ambayo amesema yanasaidia pia kuitangaza Tanzania ughaibuni.











Related Posts