HILI ni moja ya maswali ambayo pengine kwa wadau wa soka la wanawake wanalo jibu juu ya mwenendo wa mabingwa wa kihistoria, Mlandizi Queens.
Mlandizi ndio ilikuwa timu ya kwanza kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake 2017/18 kisha baadae JKT Queens ikaipokonya na kutwaa mara mbili mfululizo.
Timu hiyo iliyopanda daraja msimu huu kutoka Ligi Daraja la Kwanza ilikochukua ubingwa, hali inavyoonekana huenda ikarudi ilipotokea kutokana na mwenendo mbaya.
Tangu msimu uanze timu hiyo haijatoka nafasi iliyopo ikiendelea kusalia mkiani na pointi moja tu iliyopata na mechi 11 zote ikipoteza.
Siyo kupoteza tu, ndiyo timu iliyoruhusu mabao mengi ikifungwa 64 na kufunga mabao matano pekee.
Zimesalia mechi sita za kutetea kusalia WPL na ili ifanye hivyo inapaswa kushinda mechi zote zilizosalia itakuwa imefikisha pointi 19 itategemea na matokeo ya timu nyingine.
v Fountain Gate (ugenini)