Vietnam. Margaret Nduta Macharia (37), raia wa Kenya aliyekamatwa mwaka 2023 nchini Vietnam na dawa za kulevya kilogramu mbili za Cocaine, anatarajiwa kunyongwa hadi kufa kesho Jumatatu Machi 17, 2025.
Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Nation, Margaret aliyepewa hukumu hiyo Machi 6, 2025 alisema alipewa mzigo huo wa dawa za kulevya na mwanaume kutoka Kenya aliyemtaja kwa jina moja la John.
Pia, taarifa hiyo inaeleza kuwa alifanikiwa kupita katika viwanja vitatu vya ndege bila kukamatwa, kabla ya kugundulika Vietnam. Viwanja hivyo ni; Jomo Kenyatta (Kenya), Bole (Ethiopia) na Hamad (Qatar).
Hata hivyo, Margaret akijitetea mahakamani nchini Vietnam alidai hakufahamu kama mzigo ule ulikuwa ni dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Vietnam, Margaret atakula chakula chake cha mwisho kesho saa 1:30 usiku na kisha kunyongwa saa 2:30 za jioni.