VETA IMEFUNGUA FURSA KWA MAKUNDI MAALUM KUPATA UJUZI-CPA KASORE

Na Mwandishi Wetu

Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore amesema kuwa vyuo VETA vinatambua makundi mbalimbali yenye uhitaji.

Makundi yenye mahitaji maalum kwenye mikakati ya VETA yamepewa kipaumbele katika kuwapatia mafunzo ya ujuzi kwani ulemavu si kikwazo katika kupata elimu pamoja na hakuna sababu ya jamii kuwafungia ndani na badala yake watumie fursa ya kuwapeleka vyuo vya VETA kupata ujuzi nchi nzima

CPA Kasore aliyasema katika Maonesho na Kongamano la Mavazi, Nguo wakati alipukutana na Mlemavu wa Viungo Riziki Ndumba ambaye licha ya changamoto zake ameweza kusimama kwa kujiajiri katika fani ya ushonaji.

Amesema Riziki amepata mafunzo ya Ujuzi na Ufundi katika Chuo cha VETA Songea ambapo amehitimu na kuanza kujitegemea kwa kuwa na ofisi yake Mjini Songea.

Aidha amesema miaka 30 ya maadhimisho ni mafanikio pamoja na kuwafikia watu wenye mahitaji wakapata ujuzi na kuondokana changamoto zao na kuanza kufikiria kutengeneza uchumi.

Mhitimu Riziki anaishukuru VETA katika malezi na kupata ujuzi unaomsaidia katika maisha yake kwa sasa na baadae kuendeleza fani hiyo.

Amesema kuwa mategemeo yake ni kuongeza mashine na kuajiri vijana wenzake katika fani hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore (Kulia) akiteta jambo na Riziki Ndumba (kushoto), mhitimu wa Fani ya Ushonaji, Ubunifu na Teknolojia ya Nguo, kutoka Chuo Cha VETA Songea, wakati wa Mkutano na Maonesho ya Wadau wa Sekta ya Nguo na Mavazi yaliyonyika tarehe 14 Machi 2025, ukumbi wa Golden Jubilee, Dar es Salaam. Riziki Ndumba ni mjasiriamali mbunifu wa nguo anayeendesha shughuli zake mjini Songea, mkoa wa Ruvuma.

Related Posts

en English sw Swahili