Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa majina ya waliopita katika usaili wa maandishi, huku ikiwaita katika usaili wa mahojiano na vitendo kwa baadhi ya kada.
Tangazo hilo lililochapishwa Machi 14, 2025 katika tovuti ya BoT lilieleza wasailiwa waliopita katika mchujo huo wa awali wazingatie yafuatayo;
“Wasailiwa wote waliochaguliwa wanatakiwa kuzingatia muda na eneo la usaili na wanakumbushwa kufika na vyeti vyao halisi pamoja na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi,”ilieleza taarifa hiyo.
Aidha, tangazo hilo lilieleza kuwa usaili huo utafanyika ofisi za Bot,jijini Dar es Salaam Machi 21, 24 na 25 kulingana na kada husika ilivyopangiwa.