WASIRA:NI MARUFUKU KUWATOZA FEDHA WANAOKWENDA KUJIFUNGUA HOSPITALINI

Na Mwandishi Wetu

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepiga marufuku akina mama wajawazito wanaokwenda kujifungua hospitalini kutozwa fedha kwani huduma ya kujifungua ni bure na maelekezo tayari yalishatolewa.

Akizungumza mbele ya wananchi wa Mlowo katika Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe akiwa katika ziara yake ya kikazi Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Stephen Wasira amesema sera ya CCM inaeleza wazi huduma ya kujifungua pamoja na watoto wenye umri kuanzia mwaka 0-5 hawatatozwa fedha ,hivyo ni marufuku kuwatoza fedha.

Akiwa katika eneo hilo Wasira alipokea kero za wananchi hao wakidai wanawake wajawazito wanapokwenda kujifungua wanatakiwa kulipa fedha Sh.300,000 ili kupata huduma ya kujifungua hali iliyomshangaza na kutoa maelekezo ya kupiga marufuku huduma ya kujifungua kutozwa fedha.

“Sera ya CCM iko wazi kabisa kuwa hairuhusiwi mama mjamzito anapokwenda kujifungua kulipa fedha ili apate huduma,hivyo wale ambao wanapisha sera hii waache mara moja na hii ni kwa maeneo yote ambayo wanaendelea kupindisha utaratibu uliopo kwa kuchukua fedha.

“Watoto ni baraka na wala sio dhambi,kwanini mama anapokwenda kujifungua atoe fedha,nitoe maelekezo kwa wenyeviti wa Chama Wilaya na Mkoa kufuatilia haya yanayosemwa kama ni kweli, tuchukue hatua na nisisitize huduma ya kujifungua ni bure.”

Wasira amesisitiza suala la kina mama kujifungua bila malipo mi sera ya CCM na hiyo haina mjadala wala haina tarehe ya kuanza maana tarehe ya kuanza ilishapita nyuma.

“Kuna mambo mawili, kwanza tunataka kinamama wote wajifungue bila masharti yoyote la pili tunataka watoto wadogo kuanzia mwaka sulfuric hadi miaka mitano wapate huduma bure, kwa hiyo wale ambao wanatoza hela…kujifungua sio adhabu kama ingekuwa adhabu sote tusingezaliwa.

“Kwa sababu jambo hili ni la CCM tunaagiza uongozi wa mkoa wa Songwe na kila mahali kuhakikisha watoto na akinamama wanaokwenda kujifungua wanapewa heshima wannayostahili na hawaliposhwi fedha,” amesema.

 

Related Posts