Adebayor wa Singida BS atoswa Niger

Winga wa Singida Black Stars, Victorien Adebayor hatokuwa miongoni mwa nyota 25 wa Niger wanaoingia kambini wiki hii kujiandaa na mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Morocco.

Mchezo huo umepangwa kufanyika Machi 21, 2025 katika Uwanja wa Honor jijini Oujda, Morocco kuanzia saa 6:30 usiku.

Kuachwa huko kwa Adebayor kunamfanya atimize miezi sita ambayo amekuwa nje ya kikosi cha Niger tangu alipokitumikia mara ya mwisho, Septemba 09, 2024.

Kocha wa Niger, Badou Ezaki ameita kikosi chenye mchanganyiko wa wachezaji wanaocheza soka la kulipwa ndani ya Afrika na wengine wakiwa wanachezea klabu tofauti barani Ulaya.

Kikosi hicho kinaundwa na makipa Habiboulaye Hainikoye (US Gendarmerie Nationale), Mahamdou Tanja (AS Forces Armées Nigériennes), Babari Yahaya (US Gendarmerie Nationale).

Mabeki waliochaguliwa katika kikosi hicho ni Mohamed Abdramane (AS Douanes), Abdel-Rahim Alhassane (Real Oviedo, Spain), Aboubacar Camara (FK Bylis, Albania), Abdoulnasser Garba (US Gendarmerie Nationale) na Abraham Adamou Gora (US Gendarmerie Nationale),

Pia kuna Mame Abdoul Jalil (AS Douanes), Abdoulaye Katakore (Al Entesar, Saudi Arabia), David Lebne (AS Forces Armées Nigériennes), Oumar Sako (Rostov, Russia).

Viungo waliochaguliwa ni Ousseini Badamassi (TP Mazembe, DR Congo), Abdoulmoumouni Darenkoum (Al Mesaimeer, Qatar), Ali Mohamed (Maccabi Haifa, Israel), Harouna Moussa Hasssane (AS Forces Armées Nigériennes), Moussa Kassa (US Gendarmerie Nationale), Youssouf Oumarou (Al Karma, Iraq) na Abdoulmajid Soumana (Al Shorta, Iraq).

Kikosi hicho kinaundwa na washambuliaji Djibrill Goumey (AS Douanes), Zakariyaou Ibrahim (Gazelle, Cameroon), Djibrilla Issa (Zira, Azerbaijan), Amoustapha Kairou (Hamrun Spartans, Malta), Chamssidine Lukmane (AS Forces Armées Nigériennes) na Daniel Sosah (Kryvbas Kryvyi Rig, Ukraine)

Related Posts