CCM YAAHIDI KUENDELEA KUMUENZI DK.MAGUFULI,KUCHANGIA MILIONI 50 KUKAMILISHA UJENZI WA KANISA CHATO

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara John Mongella ameshiriki Ibada ya Shukrani ya kumbukizi ya miaka minne ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Magufuli, aliyefariki dunia Machi 17 mwaka 2021.

Akiwasilisha salamu za CCM kwa niaba ya Katibu Mkuu, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, leo Machi 17,2025 Mongella amesema kuwa Chama kitaendelea kumuenzi Hayati Dkt. Magufuli kwa kazi kubwa aliyoifanya katika ujenzi wa Taifa na ustawi wa Chama.

Wakati huo huo katika harambee ya kumalizia ujenzi wa Kanisa la Katoliki Chato, Geita, Mongella ametangaza kuwa CCM itachangia Shilingi milioni 50 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kanisa hilo, ambalo ni miongoni mwa miradi iliyoasisiwa na Hayati Magufuli.





Related Posts