KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Kibu Dennis ambaye ni maarufu kwa jina la mkandaji alipitisha mwaka mzima bila kufunga ndani ya ligi kwenye mechi za ushindani ambapo mara ya mwisho alifanya hivyo msimu wa 2023/24 jambo ambalo lilikuwa ni gumzo kubwa.
Ikumbukwe kwamba nyota huyo ambaye ni chaguo la kwanza katika kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids mara ya mwisho kufunga kwenye ligi ilikuwa ni Novemba 5 2023.
Novemba 5 2024 alitimiza mwaka mmoja bila kufunga bao lolote kwenye mechi ambazo alipata nafasi ya kucheza kwenye ligi ambapo mchezo wake wa mwisho kufunga baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 1-5 Yanga.
Gundu la Kariakoo Dabi, rasmi limeyeyuka Machi 14 2025 baada ya kufunga mabao mawili kwenye mchezo huo na ubao wa Uwanja wa KMC ulisoma Simba 6-0 Dodoma Jiji.
Katika mchezo huo Kibu alifungua akaunti ya mabao ndani ya msimu wa 2024/25 akifunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao akihusika kwenye mabao manne kati ya sita ambayo yalifungwa na Simba iliyokomba pointi tatu mazima.
Ndani ya msimu wa 2024/25 Dodoma Jiji imepoteza point izote sita mazima mbele ya Simba ambapo kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza ilikuwa Dodoma Jiji 0-1 Simba bao likifungwa na Jean Ahoua kwa mkwaju wa penati.
Mzunguko wa pili, Ahoua alitupia mabao mawili hivyo jumla kaifunga Dodoma Jiji mabao matatu kwenye mabao 12 ambayo anayo kibindoni na yote akiwa ametupia kwa mguu wa kulia.
Kibu baada ya kufunga alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo ikiwa ni tuzo yake ya kwanza ndani ya msimu ambapo aliweka wazi kuwa ni furaha kwake kuchaguliwa kuwa mchezaji bora.
“Nimefurahi kuwa mchezaji bora, shukrani kwa mashabiki haikuwa kazi rahisi hasa ukizingatia kwamba kila mchezaji anafanya kazi yake uwanjani kwenye kutimiza majukumu yake.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.