Suluhisho la Msongamano wa Bandari ya Dar – Video – Global Publishers



Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo miradi inayotekelezwa na Serikali ya Awamu Sita Machi 16, 2025, katika Bandari Kavu ya Kwala, mkoani Pwani.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema Serikali imejenga Bandari ya Kwala ili kuhimili msongamano uliopo katika Bandari ya Dar es Salaam.

Amesema kwa mwaka bandari hiyo itakuwa ikihudumia kontena 300, 000 na tangu mradi huo uanze kontena 800 zimehudumiwa, na mpaka sasa kontena 400 zimeishatolewa kwenye bandari hiyo kwenda nchi jirani za Rwanda, Malawi , Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Msigwa ameeleza hayo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari katika eneo la Bandari Kavu ya Kwala iliyopo mkoani Pwani.

 

Amesema kutokana na maboresho ya bandari hiyo, msongamano katika Bandari ya Dar es Salaam umepungua kwa asilimia 30.

Zaidi shilingi bilioni 83 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa Bandari ya Kwala ili kurahisisha utoaji wa huduma kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

Kuhusu mradi wa barabara ya Express Way kutoka Kibaha – Chalinze, Msigwa ameeleza kuwa mradi huo upo kwenye hatua za awali za utekelezaji.

 












Related Posts