ABC haitanii na imetoa fursa kwa vijana kujiunga na timu hiyo ikiwamo kupata nafasi ya kwenda mafunzo ya jeshi.
Timu hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Wanainchi wa Tanzania na inayoshiriki Ligi ya Mpira wa Kikapu Dar es Salaam (BDL) imenasa baadhi ya nyota wa ligi hiyowakiwamo Fotius Ngaiza (Vijana City Bulls) Stanley Mtungula (Dar City) , Amin Mkosa, Meshack Edward (Mchenga Star) , Baraka Sabibi (UDSM Outsiders) wakiwa uwanjani hapo.
Nyota hao waliungana na wachezaji wengine 70 kutoka Pwani na Dar es Salaam na usahili wa kwanza ulihusisha wachezaji waliocheza wenyewe kwa wenyewe.
Hata hivyo, wachezaji watakaopita walielezwa watapigiwa simu ya kuitwa katika usahili wa mwisho utakaofanyika Mkoa wa Morogoro.
Mkosa mmoja wa wachezaji tegemeo wa Mchenga Star, alisema ameamua kutafuta nafasi ya jeshi kwa lengo la kupata ajira ya kudumu.
“Mpaka sasa tunasubiri simu ya kuitwa katika usahili wa mwisho, Jeshi la Wananchi wanakuchukua kutokana na vigezo walivyoviweka,” alisema Mkosa.