BODI YA WAKURUGENZI YA TAWA YAANZA KIKAO CHAKE MKOANI MBEYA

Na Beatus Maganja, Mbeya.

Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA imekutana leo Machi 18, 2025 Jijini Mbeya Kwa ajili ya kuanza kikao chake cha Kawaida cha 30 cha Bodi hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Meja  Jenerali (Mstaafu) Hamis R. Semfuko.

Katika kikao cha siku ya Kwanza (Leo) wajumbe wa kamati za Sera, Mipango na Fedha inayoongozwa na Dr. Simon Mduma na kamati ya Ulinzi wa Rasilimali ya Wanyamapori na Uendeshaji na Usimamizi wa Rasilimali watu inayoongozwa na Prof. Jafari Kideghesho wamekutana  na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Maendeleo na ustawi wa Taasisi hiyo.

Aidha kikao hicho kinatarajiwa kufanyika Kwa siku nne ambapo Bodi itapata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Mpanga/Kipengere na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miundombinu ya utalii, miradi inayotekelezwa na TAWA hifadhini humo.

Related Posts