Bodi ya Ligi: Kama Yanga wameenda CAS ni kichekesho

Sakata la kuahirishwa kwa mechi ya Dabi ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba, iliyokuwa ichezwe Machi 8, 2025, limechukua sura mpya. Awali, suala hili lilionekana kama masihara, lakini sasa linaonekana kuingia katika hatua nzito.

Mwananchi Digital imebaini kuwa Yanga imewasilisha rasmi kesi hiyo katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) jijini Lausanne, Uswisi, baada ya kutoridhishwa na majibu ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). 


BODI YA LIGI: KAMA YANGA WAMEENDA CAS NI KICHEKESHO

Licha ya hatua hiyo, hakuna kiongozi yeyote aliyekubali kunukuliwa kwa jina, wakidai kuhofia mamlaka za soka na serikali. Hata hivyo, inadaiwa kuwa CAS itawasiliana rasmi na TFF pamoja na Bodi ya Ligi ili kuthibitisha kupokea rufaa hiyo.

Yanga inasisitiza kuwa haijaridhika na maamuzi ya ndani, hivyo imechukua hatua hiyo kutafuta haki kwenye chombo cha juu zaidi cha usuluhishi wa michezo duniani. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Steven Mnguto, amesema tayari wamejibu barua ya Yanga na hawana mamlaka ya kuwazuia kwenda CAS lakini kama wameenda CAS kwa kipindi hiki ambapo hawajasema kuwa hilo suala limeamriwa vipi itakuwa ni kitu cha kuchekesha, akisisitiza kuwa maamuzi ya mwisho ya bodi bado hayajatolewa, akiamini kuwa suluhu inaweza kupatikana kupitia vikao vya ndani.

Ameeleza kuwa busara na hekima zinapaswa kutumika ili kila upande uridhike badala ya kupeleka suala hilo nje ya nchi.

Related Posts