CHANDE : TUSISHAWISHIWE KUVUNJA AMANI YETU, NI CHACHU YA MAENDELEO

 

Mwandishi Wetu, Morogoro

NAIBU Waziri wa Fedha ,Hamad Hassan Chande amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeifungua nchi kidiplomasia ya kimataifa ambapo kwa sasa kuna maombi yapatayo 15 kutoka mataifa mbalimbali yakihitaji kuja kufanya mikutano ya kimataifa kutokana  na utulivu na amani iliyopo nchini.

 Chande amesema hayo  wakati wa hafla ya iftar iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM).

Naibu Waziri amesema Tanzania imekuwa ni kimbilio la nchi zote za Afrika sio tu Afrika Mashariki na kati bali nan chi nyingine Duniani ambazo zinataka kuja kufanya mikutano ya kimataifa kutokana na hali ya amani na utulivu.

“ Ninapo zungumza haoa tuna maombi zaidi ya 15 kwa mikutano ya kimataifa wanataka ifanyika nchini mwetu Tanzania …unafiriki ni kazi rahisi na hivi karibuni ulishafanyika mkutano wa kimataifa wa nishati safi na karibu marais 27 walifika ” amesema Chande.

 “ Na h ii si bure ni kwa sababu ya amani iliyopo na nchi yetu tumempata kiongozi miongoni mwetu ambaye na yeye anadhamini na kuimalisha  amani yetu “ amesema Chande.

Kwa msingi huo amewataka watanzania kuendelea kulinda amani na utulivu hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu kwani Mungu ameipatia neema kubwa ya kuwa amani na utulivu hivyo ni vyema kuithamini kwa kiwango kikubwa.

“ Leo wenzetu nchi jirani wanashindwa kufanya ibada kama hizi kwa wazi na utulivu kwa sababu hakuna amani na utulivu , ni vyema watanzania tuwaepuke watu wanaoshawishi kuvunja amani ya nchi yetu” amesema Chande.

Naibu Waziri amesema katika kipindi hiki tunachoelekea kwenye uchaguzi tunapaswa kuwa wamoja bila ya kujali dini zetu, makabila yetu wala itikadi zetu za siasa, kwani tukianza kuharibu amani yetu mjue tunawapa nafasi wabaya wetu wasiotutakia mema.

Katika hatua nyingine amewataka Wanafunzi wa vyuo Vikuu kutumia hotuba za Rais Dk Samia Suluhu Hassan kufanya tafiti mbalimbali za kiuchumi na maendeleo yaliyofikiwa.

Naibu Waziri Chande amesemakuwa wanafunzi hao wanaweza kutumia hotuba hizo kufanyia utafiti na rejea kwenye masomo yao na hivyo kuitangaza Tanzania .

Kwa upande wake Sheikh wa mkoa wa Morogoro Twaha Kilango amesema waislamu wa mkoa wa Morogoro wamepanga kufanya dua kwa ajili ya kuliombea Taifa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Kilango amewataka  waislamu kufanya ibada ya funga kwa kuwa imeamrishwa na mwenyezi Mungu huku akiwaonya waislamu kuepuka matendo yanayowakera wengine katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyoshiriki ifrari hiyo kiongozi wa serikali ya wanafunzi wa  MUM  ,Adam Hamis alisema lengo la Chuo  kuandaa Ifrari hiyo ni kujumuika na wanafunzi wenzao WA  vyuo vingine vikiwemo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) , Chuo Kikuu Mzumbe na vingine  vya Morogoro ,pia kuliombea Taifa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu .Naibu Waziri wa Fedha ,Hamad Hassan Chande ( watatu kutoka kulia) akiwa na baadhi ya waumini  na wadau wengine walioalikwa kushiriki hafla ya iftar iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM).

Related Posts