Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, Marry Sule amefariki dunia jana usiku Machi 18, 2025 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Huruma.
Taarifa za kifo chake zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii usiku huohuo zikieleza kuwa Katibu huyo amefariki muda mfupi baada ya kutoka kwenye chumba cha upasuaji kwenye Hospitali ya Huruma, iliyopo wilayani humo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rombo, Antony Tesha amethibitisha kutokea kwa kifo hicho.
“Nasikitika kutangaza kifo cha Katibu wa CCM Wilaya, ndugu Mary Sule kilichotokea jana usiku katika Hospitali ya Huruma alikokuwa akipatiwa matibabu,”imeeleza taarifa hiyo iliyotolewa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rombo
Endelea kufuatilia mitandao yetu kwa habari zaidi.