MADAKTARI BINGWA WA MAMA SAMIA WATOA MAFUNZO YA UTOAJI HUDUMA KWA MAMA NA MTOTO

Madaktari bingwa wa mpango wa Mama Samia kutoka mikoa mbalimbali wametoa mafunzo ya kuboresha utoaji huduma kwa mama na watoto wachanga kwa watumishi wa afya wa Hospitali ya Wilaya ya Singida na vituo vya afya jirani.

Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo watoa huduma, hasa katika sekta ya afya ya mama na mtoto, ili kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga. Mafunzo hayo ya siku tatu yalifanyika kuanzia tarehe 17 hadi 19 Machi, 2025, katika ukumbi wa Hospitali ya Wilaya ya Singida.

Watumishi wa afya walioshiriki wameeleza shukrani zao kwa madaktari hao kwa ujuzi waliopata na wameahidi kutumia maarifa hayo kuboresha utoaji huduma na kuongeza weledi katika kazi zao za kila siku.

Mpango huu ni moja ya juhudi za serikali za kuimarisha huduma za afya nchini na kuhakikisha mama na mtoto wanapata huduma bora na salama.







Related Posts