Sheikh Njalambaha aonya fikra mbaya kuelekea Uchaguzi Mkuu

Mbeya. Viongozi wa dini ya Kiislamu Mkoa wa Mbeya wamefanya dua maalumu ya kuliombea Taifa na viongozi  wa Serikali akiwepo Rais Samia Suluhu Hassan katika  kuelekea uchaguzi Mkuu Oktoba 2025.

Mbali na dua hilo wakikemea baadhi ya Watanzania kujiepusha na fikra mbaya za kujihusisha uvunjifu  wa amani na badala yake kuombea  utulivu na amani kwa maslai ya Watanzania na Taifa kwa ujumla.

Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Msafiri Njalambaha ametoa kauli hiyo leo Jumatano Machi 19, 2025 baada ya kufanya dua maalumu na kupokea futari za wahitaji 200   iliyotolewa na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kupitia Taasisi ya Tulia Trust.

Njalambaha amesema huu ni mwaka wa uchaguzi  kama viongozi wa dini wanalojukumu kubwa kuungana na waumini na Watanzania kuombea amani, utulivu na  kukemea vitendo viovu.

“Taifa letu limepata tunu ya viongozi wa ngazi za  juu  wanawake akiwepo Rais Samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya, Dk Tulia Ackson, hivyo niwaombe Watanzania tuzitunze hizi tunu na tusikubali kuzipoteza,” amesema.

Wakati huo huo,Shekhe Njalambaha amewataka wananchi kutohusisha misaada inayotolewa na Mbunge wa Mbeya mjini, Dk Tulia Ackson na  masuala ya kisiasa kutokana na kuelekea kipindi  cha  uchaguzi.

“Hii siyo mara ya kwanza kiongozi huyo kugusa wahitaji kila mwaka anatoa mahitaji katika kipindi cha mfungo wa Idd  El-Fitr, niombe tu waumini na Watanzania kuendelea kumuombea na kuliombea Taifa akiwamo Rais Samia Suluhu Hassan,” amesema.

Meneja wa Taasisi ya Tulia Trust ,Jackline Boaz(kushoto) akikabidhi futari kwa Shekhe wa Mkoa wa Mbeya, Msafiri Njalambaha (kulia) kwa ajili ya wahitaji 200. Picha na Hawa Mathias

Amesema matendo yanayofanywa, Dk Tulia kuigusa jamii ya Kimungu na siyo mara ya kwanza kugusa wahitaji.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Baraza la Masheikhe Mkoa, Sheikh Ibrahim Bombo ameishukuru Taasisi ya Tulia Trust kwa utaratibu wake wa kugusa walengwa huku akiwataka maimamu wa misikiti iliyoguswa  kuhakikisha walengwa wanafikiwa.

” Tuna kila sababu ya kushukuru kwa mahitaji ya  walengwa 200 katika misikiti mbalimbali katika Jiji la Mbeya,  jukumu letu ni kuendelea kufanya dua kumuombea,” amesema.

Mwakilishi wa Taasisi ya Tulia Trust, Athuman Kapuya ameshukuru ushirikiano wa viongozi wa dini na kuomba kuendelea kumuombea Spika wa Bunge na Mbunge Mbeya Mjini, Dk Tulia Ackson.

Amesema wataendeleza ushirikiano unaogusa jamii yenye mahitaji katika mfungo na  kuelekea Sikukuu ya Idd.

Mnufaika Stumahi Michuzi amesema wataendelea kufanya dua kumuombe Mbunge wa Mbeya, Dk Tulia,  Mungu aendelee kumzidishia kutokana na namna anavyojitoa kugusa jamii yenye uhitaji.

Related Posts