Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw Hamza Saidi Johari jana aliongoza mamia ya Waislamu ambao ni wateja wa benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwenye hafla fupi ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo huku akisisitiza umuhimu wa taasisi za fedha nchini kuzingatia mahusiano na huduma zinazo heshimu sheria, imani na misingi ya dini za wateja.
Hafla hiyo ilifanyika jana kwenye hotel ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam ikihudhuriwa pia na viongozi wa dini, viongozi wa serikali pamoja na wateja wa benki hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC Bw Theobald Sabi aliwaongoza wafanyakazi wengine wa benki hiyo kwenye hafla hiyo.
Katika hotuba yake, Bw Johari pamoja na kuipongeza benki ya NBC kwa ushirikiano wake na wadau wake alisisitiza umuhimu wa mahusiano yanayogusa na kuheshimu misingi ya imani za dini kwa wateja wa taasisi mbalimbali za kifedha nchini kwa kuwa pamoja na kuboresha mahusiano zaidi, hatua hiyo inatoa wasaa na kuhamasisha idadi kubwa ya wateja ambao wanashindwa kushirikiana na taasisi hizo wakihofia huduma zenye ukiukwaji wa misingi ya imani zao za kidini.
“Mahusiano ya namna hii yanasaidia kuchochea uchumi jumuishi zaidi kwa kuwa sasa benki zinajipambanua kama mshirika muhimu kwa wateja si tu kwa malengo ya usalama wa fedha zao na sababu za kiuchumi bali wateja wanahisi wapo mikono salama hata kiimani kwa kuwa wanapata wasaa wa kushiriki nanyi pamoja kwenye masuala yanayohusu imani zao na zaidi wanapata nafasi kusikia huduma mbalimbali za kifedha zilizobuniwa kwa kuzingatia misingi imani zao za kidini…hongereni sana,’’ alisema.
Kwa upande wake Bw Sabi alisema benki hiyo imekuwa ikiutambua mwezi wa Ramadhani kuwa ni nguzo muhimu ya imani ya Kiislamu, wakati wa ibada, upendo, na sadaka hivyo imekuwa ikiutumia kama ishara yake ya msingi katika kuthibitisha mahusiano yake na wateja pamoja na wadau wote wa benki hiyo ikiwemo serikali lengo likiwa ni kushirikiana pamoja baraka za mwezi huo.
“Hivyo kipekee kabisa niwashukuru nyote kwa kuendelea kuiamini Benki ya NBC kama mshirika wenu wa kifedha. Tunaahidi kuendelea kuboresha huduma zetu, ikiwemo akaunti za La Riba zinazofuata taratibu za ‘Sharia’ ili kufikia mahitaji yenu ya kibenki. Nichukue pia fursa hii kuwakaribisha kutumia huduma yetu iliyoboreshwa ya ‘NBC Kiganjani’ ambayo ni huduma ya kibenki kwa simu za mkononi.’’ Alisema.
Akifafanua zaidi kuhusu NBC Kiganjani iliyoboreshwa Sabi alisema: “Kupitia NBC Kiganjani sasa mteja anaweza kufungua akaunti yeye mwenyewe, kufanya malipo ya serikali (GEPG), kununua LUKU, na kufanya malipo kupitia NBC Lipa Namba na huduma mpya ya Edu-Connect kwa ajili ya malipo ya ada za shule’’
Hafla hiyo pia ilihusisha utoaji wa zawadi kwa wageni waalikwa. Kwa wateja wa Kiislamu wa benki ya NBC jijini Dar es Salaam, hafla hiyo ilikuwa fursa nzuri ya kufurahi pamoja na kujenga uhusiano mzuri miongoni mwao na benki hiyo.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw Hamza Saidi Johari (kushoto) akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC Bw Theobald Sabi (kulia) wakati wa hafla futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam jana . Hafla hiyo ilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw Hamza Saidi Johari (kulia) akiwaongoza wageni waalikwa kupata futari wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam jana. Hafla hiyo ilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC Bw Theobald Sabi (kulia) akiambatana na wageni waalikwa kupata futari wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam jana. Hafla hiyo ilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC Bw Theobald Sabi (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sheikh Adam Mwinyipingu (pichani) akiongoza Dua maalum mbele ya wageni waalikwa wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC Bw Theobald Sabi (kushoto) akibadilishana mawazo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw Hamza Saidi Johari wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw Hamza Saidi Johari (Katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa pili kushoto walioketi) wakati wa hafla futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam jana . Pamoja nao yupo Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sheikh Adam Mwinyipingu (wa pili kulia walioketi). Hafla hiyo ilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa dini, wateja, viongozi wa serikali, wafanyakazi na viongozi waandamizi wa benki ya NBC,