KIPA Mzambia Toaster Nsabata ambaye raia wa Zambia anayekipiga Zesco Utd na Msauzi Xolani Ngcobo wa Klabu ya Royal AM ya nchini huko ni kati ya majina yanayoshindanishwa na Kipa wa Yanga, Djigui Diarra katika kikosi cha Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
Kati ya makipa hao mmoja wao anatarajiwa kusajiliwa na Kaizer Ciefs katika usajili wa msim ujao, licha ya Diarra kupewa nafasi kubwa ya kusajiliwa ndani ya kikosi hicho.
Kwa mujibu wa Chanzo cha Habari kutoka ndani ya Yanga, tayari Kaizer Chiefs wameulizia uwezekano wa kumpata Diarra katika msimu ujao ambaye yupo katika kiwango bora.