KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Jean Charles Ahoua anaongoza orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 12, huku ligi timuhiyo ikisaliwa na mechi nane kufunga msimu na kuwa na kibarua kizito cha kuifikia rekodi iliyowahi kuwekwa na Meddie Kagere akiwa anaitumikia timu hiyo.
Kagere aliandika rekodi ya kuwa nyota wa kigeni aliyefunga mabao mengi zaidi katika Ligi Kuu akitupia 23 msimu wa 2018-2019 ambayo hata mwenyewe alishindwa kuifikia licha ya kutetea Kiatu cha Dhahabu msimu uliofuata wa 2019-2020. Kwa sasa Kagere anakipiga Namungo inayonolewa na kocha Juma Mgunda.
Imeshapita misimu saba tangu rekodi hiyo iwekwe na Kagere, huku hakuna nyota yoyote wa kigeni aliyeifikia akiwamo Kagere mwenyewe, kwani msimu uliopita Stephane Aziz KI wa Yanga akijitutumua na kufikisha mabao 21 kama ayaliyowahi kuwekwa na Amissi Tambwe alipokuwa Yanga msimu wa 2015-2016.
Kazi sasa imehamia kwa Ahoua mwenye mabao 12, yakiwamo matano ya penaltikupitia mechi 21, akianza 17 na nne akitokea benchi huku akiwa na asisti sita hadi sasa.
Kitakwimu, Ahoua ana wastani wa kufunga bao moja katika mechi mbili, hivyo kwa mechi zilizosalia anaweza akafunga manne tu, kitu kinachompa ugumu kuifikia rekodi ya Kagere.
Kagere alicheza misimu minne Simba alifunga jumla ya mabao 65, ambapo 2018/19 (23), 2019/20 (22), 2020/21 (13) na 2021/22 (7).
Hata hivyo, kocha Fadlu Davids anaamini uwezo wa washambuliaji wa Simba, akiwamo Ahoua kuwa watafunga mabao mengi, ila baadhi ya mastaa wa zamani wanaona kuifikia au kuivunja rekodi ya Kagere kwa msimu huu nui ngumu kwa mechi zilizosalia.

Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ aliyeshikilia rekodi ya mabao 26 ya mwaka 1998, alisema kwa msimu huu haoni mchezaji wa kufikisha mabao 23 ya Kagere.
“Kuna rekodi nyingi za mabao, mfano ili mchezaji aifikie yangu atatakiwa aanze na ya Abdallah Juma aliyefunga 25 aliyofunga 2006 ndipo zifuate nyingine,” alisema Chinga, huku Juma akikazia:”Wachezaji wa sasa wakiamua kupambana wanaweza, kama Kagere.”