Ama kweli kabla haujafa, haujaumbika! huyu ni Ramadhan, kijana mwenye umri wa miaka 17, ambaye kutokana na tatizo lake la kiafya, ameshindwa kuwa kama vijana wengine wa rika lake, kielimu na katika maendeleo ya kimwili.
Ramadhan amekatishwa ndoto zake za kusoma baada ya ngozi yake kuota hadi usoni, jambo lililomfanya apitie maumivu makali kila siku. Licha ya hali hiyo, bado anaonesha moyo wa matumaini na tabasamu.
Mtayarishaji wa maudhui, @zali_mapito, amefika nyumbani kwa Ramadhan na kuzungumza naye pamoja na mama yake, ambaye amewaomba Watanzania wamsaidie kijana wake ili aweze kupata matibabu.
Kiasi kinachohitajika kwa ajili ya upasuaji unaoweza kumrejesha shuleni na kurudisha uwezo wa kuona ni shilingi milioni 7 tu.
Wote wenye moyo wa kusaidia wanakaribishwa kujitokeza ili kuokoa maisha ya Ramadhan na kumpa fursa ya kuishi kama kijana mwingine yeyote.