MSD YABAINISHA KUONGEZEKA KWA BIDHAA ZA AFYA ASHIRIA KUTOKA 290 HADI 382.

Na Mwandishi wetu Dodoma.

MKURUGENZI Mkuu Bohari ya Dawa (MSD) Mavere Tukai amesema kuwa kutokana na nia ya Serikali kuboresha maisha ya Watanzania kuanzia mwaka wa fedha 2023/24 idadi ya bidhaa ashiria zinazotumika kupima hali ya upimaji wa bidha za Afya zimeongezeka kutoka bidhaa 290 hadi kufikia bidhaa 382.

Tukai ameyasema hayo leo hii Jijini Dodoma Machi 19,2025 wakati akizungumza na Wanahabari akielezea mafanikio ya Taasisi hiyo katika Maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita.

Amesema kuwa hali ya uwepo wa bidhaa za afya ashiria 382 imeongezeka kutoka asilimia 42 mwaka 2021/22 hadi kufikia asilimia 67 mwezi Februari 2024/25 sawa na ongezeko la asilimia 23, na kufanya hali ya upatikanaji wa bidhaa za afya kuimarika mwaka hadi mwaka.

“Bohari ya Dawa imeendelea kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya katika vituo vya kutolea huduma za afya. Uwepo wa bidhaa za afya umekuwa ukipimwa kwa bidhaa za afya ashiria 290, lakini kutokana na kuimarisha mifumo ya utoaji huduma na nia ya Serikali ya kuboresha maisha ya Watanzania kuanzia mwaka wa fedha 2023/24 idadi ya bidhaa ashiria zinazotumika kupima hali ya upimaji wa bidhaa za afya zimeongezeka kutoka bidhaa 290 hadi kufikia bidhaa 382”. Amesemq

Aidha ameeleza kuwa katika kipindi cha Serikali ya awamu ya sita vituo vya kutolea huduma za afya vinavyohudumiwa na MSD vimeongezeka na kufikia vituo 8,466 mwaka 2024/25 kutoka vituo 7,095 mwaka 2021/22 sawa na ongezeko la vituo 1,371 ikiwa ni ongezeko la asilimia 19.

Mbali na hayo pia amesema kuwa katika kuboresha afya ya Mama na Mtoto Serikali kupitia Bohari ya Dawa katika miaka minne imenunua na kusambaza bidhaa za afya kwaajili ya kuboresha vituo vya afya 316 na kuhakikisha vinatoa huduma ya dharura ya uzazi na mtoto ambapo bidhaa zote za afya 414 zenye thamani ya Shilingi 100,182,390,897.40 zimekwisha sambazwa na kusimikwa kwenye vituo hivyo vya kutolea huduma za afya Nchini.

Bohari ya Dawa (MSD) ni Taasisi ya inayomilikiwa na Serikali iliyoanzishwa mwaka 1993 kwa mujibu wa Sheria Bohari ya Dawa Na.13.  

Related Posts