NMB Yaendeleza Utamaduni wa Futari ya Kipekee kwa watoto vituo vitano na Wabunge Dodoma

Na Mwandishi Maalum

Moja ya matukio makubwa nchini wakati jua linazama Jumatano wiki hii ilikuwa ni futari ya kukata na shoka iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa ajili ya watoto waishio katika mazingira magumu pamoja na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika kuendeleza jadi yake ya kutoa misaada ya kijamii, Benki ya NMB ilitwakusanya watoto kutoka vituo vitano vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu vya Ghadaf, Arrahman, Imam Swadiq, Ndachi, na Zam Zam katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Watoto hawa walishiriki futari na wadau wa NMB na pia walipokea mahitaji muhimu ya chakula na vifaa vya matumizi ya kila siku, jambo lililodhihirisha dhamira ya benki hiyo katika kusaidia jamii zenye uhitaji

Wengi wa wadau waliohudhuria tukio hilo katika Viwanja vya Bunge walisema kufanyika na kufana kwake ni mwendekezo wa desturi ya NMB ya kila mwaka ya kushiriki baraka za Ramadhani kwa wenye uhitaji na wadau wake wakuu.

Wakitoa pongezi kwa benki hiyo kwa kubadilisha futari hizo kutoka kuwa tukio la kawaida la kufuturu hadi kuwa jukwaa lenye tija, wabunge waliohojiwa wamebainisha kuwa hafla hizo sasa zinahamasisha zaidi kubadilishana mawazo na uzoefu wa mambo mablimbali pamoja na kuchochea mijadala ya ustawi na maendeleo ya taifa.

“Futari hizi sasa zimekuwa tukio muhimu kwenye kalenda ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani nchini, zikithibitisha dhamira ya NMB katika kuimarisha mahusiano na wadau wake huku zikichangia katika ujenzi wa taifa, alisema Mbunge wa Njombe Mjini, Mhe. Deo Mwanyika.

Kwa upande wake, Mbunge wa Makete, Bw. Festo Richard Sanga, pia alipongeza ukarimu wa benki hiyo na kueleza kuwa hafla hizi zimekuwa maarufu hata katika kukumbushia kuwakumbuka wenye uhitaji lakini pia kuimarisha mshikamano.

“Futari ya zinazoandaliwa na Benki ya NMB kwa ajili ya watoto hawa pamoja na Wabunge zinaendelea kuwa alama ya umoja, ukarimu, na ushirikiano wenye tija, ikiimarisha nafasi ya NMB kama mshirika mkuu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Tanzania,” alieleza Bw. Sanga.

Futari ya mwaka huu iliudhuriwa pia na mawaziri, manaibu waziri, maafisa waandamizi wa serikali, viongozi wa mashirika ya umma na binafsi, makamanda wa vikosi vya ulinzi na usalama, viongozi wa dini, pamoja na wateja wa benki hiyo.

Mbunge wa Viti Maalum kutoka Tabora, Bi Hawa Mwaifunga, alisema huo ni mwendekezo wa NMB kusaidia jamii na kuwa msaada huo wa kinadamu
umeleta furaha, heshima, na matumaini kwa watoto hao wanaoishi kwenye mazingira magumu.

“Mchango wa Benki ya NMB kwa watoto hawa ni mkubwa na muhimu katika malezi yao. Unawsajengea utamaduni wa ukarimu na ushirikishwaji, kuhakikisha wao nao wanajihisi kuthaminiwa na kuwa sehemu ya jamii pana,” alibainisha.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi Ruth Zaipuna, alieleza umuhimu wa Futari za NMB kwa Bunge katika kuimarisha ushirikiano kati ya benki hiyo, wabunge, na serikali kwa ujumla.

Kukaribishwa kwetu hapa mara kwa mara, inadhihirisha mahusiano mazuri ambayo Benki ya NMB inayo na Bunge lako Tukufu lakini zaidi na Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alimwambia ngeni rasmi, Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Najma Murtaza Giga.

Akizungumza kwa niaba ya Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, mgeni rasmi wa hafla hiyo Bi Najma, alieleza kuwa mafanikio makubwa ya Benki ya NMB yanatokana na fadhila za ukarimu wake na baraka za ushirikiano wa kimkakati.

Alisisitiza kuwa benki hiyo si tu kwamba inajali wenye uhitaji, bali pia inadhihirisha roho ya huduma na mshikamano, ikishirikiana kwa karibu na Bunge ili kuendeleza maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa manufaa ya taifa kwa ujumla.









 

Related Posts