SOUWASA YA PITA NYUMBA KWA NYUMBA KUHAMASISHA WATEJA WALIOSITISHIWA HUDUMA HIYO KUIREJESHA NDANI YA WIKI YA MAJI.

 Belinda Songea: NA BELINDA JOSEPH, SONGEA.

Katika kuadhimisha wiki ya maji, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Songea SOUWASA, imezindua kampeni maalumu kuelekea kilele cha wiki hiyo, kwa lengo la kuhamasisha wateja waliositishiwa huduma kulipia nusu ya deni lao na kurejeshewa huduma,  Kampeni hii imewekwa mkazo mkubwa katika kuelimisha na kuwahimiza wateja kurejesha huduma zao kwa kutumia ofa maalumu iliyotolewa na SOUWASA.

Timu maalumu ya Wataalamu wa  SOUWASA ikiongozwa na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Bi Baby Biko, ambayo  imetembelea na kupita nyumba kwa nyumba maeneo ya Ruhuwiko Kanisani na Ruhuwiko Shuleni ili kukutana na wateja na kuwaeleza kuhusu fursa hii ya kipekee, Lengo la ziara hii ni kuwahamasisha wateja kurejesha huduma zao ili waweze kufaidika na huduma bora za maji zinazotolewa na Souwasa.

Ofa hii maalumu  itadumu kwa muda wa wiki moja tu, kuanzia tarehe 16 hadi 22 Machi 2025, hivyo  Wateja waliopo katika maeneo hayo wanashauriwa kuchukua fursa hii kwa haraka kabla ya ofa kumalizika, ili waweze kuendelea kufurahia huduma za maji bila usumbufu.

SOUWASA inawashauri wateja wote walio na deni kulipia nusu ya deni lao ndani ya kipindi hiki cha wiki ya maji ili  kurejeshewa huduma zao haraka iwezekanavyo, Hii ni fursa adimu kwa wateja kurejesha huduma zao na kuendelea kufaidika na maji safi na salama, jambo muhimu kwa ustawi wa jami

Related Posts