TFF yaufungulia uwanja wa CCM Kirumba

SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF) limeufungulia Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza baada ya kufanyiwa marekebisho.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo imeeleza kuwa uwanja huo ulifungiwa kutokana na miundo mbinu hiyo kutofaa.

“Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) limeufungulia Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kutumika kwa michezo ya Ligi baada ya kufanya marekebisho yaliyokidhi vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu,”

“Uwanja huo uliofungiwa kutokana na miundombinu yake kutofaa kutumika kama ilivyoainishwa kwenye masharti ya kanuni ya leseni za klabu umekaguliwa na kukidhi vigezo vya kikanuni baada ya marekebisho yaliyoelekezwa kufanyika,”

“TFF inaendelea kuzikumbusha klabu kuendelea kuboresha na kutunza miundombinu ya viwanja vyao vya nyumbani kwa kushirikiana na wamiliki (kwa klabu ambazo hazimiliki viwanja) ili michezo ya Ligi ichezwe kwenye viwanja bora vinavyosaidia kuongeza ushindani na thamani ya ligi.”

Machi 10, 2025 Shirikisho hilo lilivifungia viwanja vitatu kwa paoja ambavyo ni Liti unaotumiwa na Singida Black Stars, Kirumba unaotumiwa na Pamba Jiji, pamoja na Jamhuri Dodoma unajotumiwa na Dodoma Jiji FC ambapo hadi sasa ni kiwanja kimoja tu kilichofunguliwa ambacho ni CCM Kirumba.

Related Posts